Habari

Wizara ya Afya yaagiza kuchunguza tukio la Bi. Esther

Wizara ya Afya imeelekeza Baraza la Famasia na Bodi ya Hospitali Binafsi kuchunguza tukio la Bi. Esther Mkombozi kuchomwa sindano katika duka la dawa huko Arusha.

Taarifa iliyotolewa na Wizara hiyo kwa Umma imeonesha kusikitishwa na Bi. Esther Mkombozi, mkazi wa Arusha, Mtaa wa Kimandolu ambave ameeleza kuwa alichomwa sindano katika duka la dawa na kumsababishia madhara katika mkono wake.

VIDEO

”Wizara ya Afya imepokea kwa masikitiko kuhusu taarifa iliyosambaa kwenye mitandao va kijamii kuanzia tarehe 07 Mei, 2023 kuhusiana na Bi. Esther Mkombozi, mkazi wa Arusha, Mtaa wa Kimandolu ambave ameeleza kuwa alichomwa sindano
katika duka la dawa na kumsababishia madhara katika mkono wake.”

”Tunapenda kuufamisha umma kuwa, ni kosa kisheria kwa duka lolote la dawa nchini kutoa huduma za kitabibu ikiwa ni pamoja na kuchoma sindano, kufanya tohara au vipimo vya kimaabara.”

”Kutokana na hilo, Wizara imeelekeza Baraza la Famasi (PC) na Bodi va Hospitali Binafsi (PHAB) kufuatilia suala hili mara moja ili hatue stahiki ziweze kuchukuliwa kwa wote watakaobainika kukiuka Sheria, Kanuni, Miongozo na Taratibu za Usimamizi na Udhibiti wa utoaji wa huduma za Afya nchini.”

”Tunampa pole Bi. Esther kutokana n madhara aliyopata. Tuwaomba wananchi kuendelea kuwa watulivu ambapo suala hili linafanyiwa kazi.”

”Wizara ya Afya inatoa wito kwa wananchi kuhakikisha wanapata huduma za afya katika maeneo stahiki ikiwemo Hospitali, Vito vya Afya na Zahanati ili kuepuka madhara a athari mbalimbali zinazoweza kuwapata ikiwa watakwenda sehemu zisizo rasmi.”

Imeandikwa na @fumo255 video credit by Gadi Tv

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents