X ndio nembo ya rasmi ya Twitter kuanzia leo

Hii ndio nembo mpya ya Twitter, X nyeupe yenye rangi nyeusi nyuma, imezinduliwa na afisa mkuu mtendaji wa Twitter, baada ya mmiliki wake Elon Musk kusema anataka kuondoa nembo ya ndege.
Katika ujumbe wake wa Twitter aliochapisha Jumatatu asubuhi, Linda Yaccarino alisema “X yuko hapa! Hebu tufanye hivi.”
Bw Musk pia alibadilisha picha yake ya wasifu na kuweka nembo mpya na kuongeza “X.com” kwenye wasifu wake wa Twitter.
Kulingana na ripoti, anataka kuunda “super app” inayoitwa “X”.
Siku ya Jumapili, bilionea huyo alisema anatazamia kubadilisha nembo ya Twitter, ambapo alituma ujumbe wa Twitter : “Na hivi karibuni tutaomba radhi kwa chapa ya Twitter na, pole pole, ndege wote.”
Alisema pia kwamba nembo ya muda ingeonyeshwa moja kwa moja baadaye siku hiyo hiyo.
Bw Musk alichapisha picha ya “X” iliyopeperushwa kwenye Twitter, na baadaye katika mazungumzo ya sauti ya Twitter Spaces, alijibu “Ndiyo” alipoulizwa ikiwa nembo ya Twitter itabadilika, akiongeza kuwa “mabadiliko haya yalipaswa kufanyika muda mrefu uliopita”.
Mtendaji mkuu wa kampuni hiyo, Linda Yaccarino, aliandika kwenye jukwaa kwamba urejeshaji wa chapa hiyo ulikuwa fursa mpya ya kusisimua.
Bwana Musk alishutumiwa kwa biashara ya ndani na kundi la wawekezaji wa Dogecoin, ambao walidai kuwa alifaidika kutokana na kuongeza thamani ya Dogecoin.
Kampuni hiyo ilikosolewa na watumiaji na wenye masoko ya mitandaoni Bw Musk alipotangaza mapema mwezi huu kwamba kutakuwa na kikomo cha idadi ya jumbe za twitter kwa siku.
Vikomo vya kila siku vya jumbe za Twitter vilisaidia katika ukuaji wa jukwa la Threads la huduma pinzani zinazomilikiwa na kampuni ya Meta, ambazo zilikuwa na usajili zaidi ya milioni 100 katika siku tano za kuzinduliwa.
Masaibu ya hivi karibuni zaidi ya witter ilikuwa ni kesi iliyowasilishwa Jumanne ambayo ilidai kuwa kampuni hiyo inadaiwa angalau $500m (£388.7m) ya malipo ya kuwasimisha kazi wafanyikazi wake zamani.
Tangu Bw Musk alipoinunua, kampuni hiyo imepunguza zaidi ya nusu ya wafanyikazi wake.