Yaelezwa udongo kutoka mwezini kukuza mimea

Wanasayansi wamepanda mimea kwenye udongo wa mwezini kwa mara ya kwanza , ikiwa ni hatua muhimu kuelekea kuishi kwa muda mrefu mwezini iwezekanavyo.
Watafiti walitumia sampuli ndogo za vumbi iliyokusanywa wakati wa safari yaApolo kati yam waka 1969-1972 Apollo kupanda aina mboga za jamii ya kabeji.
Walishangaa sana kwamba, mbegu zilianza mbegu zilianza kutoka baada ya siku mbili.
“Siwezi kukwambia jinsi tulivyoshangaa ,” alisema Anna-Lisa Paul, Profesa katika Chuo kikuu cha Florida ambaye ni mwandishi mwenza wa matokeo ya utafiti.
“Kila mmea-uwe ni wa sampuli ya mwezi au unaodhibitiwa- ilionekana sawa hadiilipofika siku ya sita baadaye.”
Baada yah apo, tofauti zilijitokeza. Mimea iliyopandwa katika udongo wa mwezini ilianza kuonyesha kunyong’onyea, ikaanza kukua kwa kurora zaidi na kuishia kudumaa.
Lakini wale waliohusika wanasema ni mafanikio- na yenye athari za kidunia.