FahamuHabari

Yafahamu mataifa 10 yanayozalisha gesi asilia kwa wingi zaidi

Gesi asilia ni gesi ya hidrokaboni inayotokea kiasili na mafuta yasiyoweza kurejeshwa ambayo hutoka chini ya uso wa Dunia. Gesi asilia hutumika kupasha joto sehemu za baridi, kupikia na kuzalisha umeme. Gesi asilia pia inaweza kutumika kama mafuta ya magari na katika utengenezaji wa plastiki. Ingawa gesi asilia bado inachangia mabadiliko ya hali ya hewa inapochomwa, pia huwaka kwa usafi zaidi kuliko nishati nyinginezo kama vile makaa ya mawe na mafuta na ndio maana mataifa mengi hasa likiwemo Tanzania yanasisitiza sana matumizi ya gesi.

Wazalishaji wengi wakubwa zaidi wa gesi asilia duniani ni makampuni makubwa ya nishati yenye shughuli za kuchimba mafuta na gesi duniani, Marekani ndiyo mzalishaji mkuu wa gesi asilia duniani ikifuatiwa na Urusi, Iran, Qatar, China na Kanada.

Kumbuka kuwa Marekani ndiyo nchi inayoongoza kwa uzalishaji wa gesi asilia duniani ikifuatiwa na Urusi, Iran, Qatar, China na Kanada.
Kampuni kubwa zaidi ya mafuta na gesi duniani kwa mapato ni China National Petroleum/PetroChina ya China.
Makampuni kumi ya juu ya gesi asilia duniani yanatoka Marekani, Urusi, Saudi Arabia, Uholanzi, China, U.K., na Ufaransa.

Haya ni mataifa yanayoongoza duniani kwa uzalishaji wa gesi asilia kulingana na jarida la

1. Marekani ikiwa na mita za ujazo bilioni 934.2  

2. Russia: ikiwa na mita za ujazo bilioni 701.7  

3. Iran: ikiwa na mita za ujazo bilioni 256.7  

4. China: ikiwa na mita za ujazo bilioni 209.2  

5. Qatar: ikiwa na mita za ujazo bilioni 177.0  

6. Canada: ikiwa na mita za ujazo bilioni 172.3  

7. Australia: ikiwa na mita za ujazo bilioni 147.2  

8. Saudi Arabia: ikiwa na mita za ujazo bilioni 117.3  

9. Norway: ikiwa na mita za ujazo bilioni 114.3  

10. Algeria: ikiwa na mita za ujazo bilioni 100.8

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents