FahamuHabari

Yafahamu matendo ambayo ni kinyume cha sheria wakati wa Sensa

Siku ya leo Ofisi ya Taifa ya Takwimu NBS imeandaa mafunzo kwa wanahabari wa mitandao ya kijamii Tanzania ili kuwajengea uelewa wanahabari hao kuhusu maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 ambayo inatarajiwa kuanza Agosti 23. Mafunzo hayo yameanza leo Juni 14, 2022 mjini Iringa na yatahitimishwa hapo kesho Juni 15.

 

Wakati mafunzo hayo yanaendelea yametajwa matendo ambayo ni kinyume cha sheria wakati wa Sensa

i. Kumzuia Karani kuchukua Taarifa.

ii. Kutoa taarifa zisizo sahihi.

iii. Kuharibu Fomu/Vitendea kazi vya karani.

iv. Kujifanya afisa wa Sensa.

v. Kumshawishi mtu kutoshiriki Sensa.

vi. Kutumia Takwimu za sensa kwa taarifa zako binafsi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents