Habari

Yafahamu maswali yatakayoulizwa katika sensa ya mwaka 2022

Siku ya leo Ofisi ya Taifa ya Takwimu NBS imeandaa mafunzo kwa wanahabari wa mitandao ya kijamii Tanzania ili kuwajengea uelewa wanahabari hao kuhusu maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 ambayo inatarajiwa kuanza Agosti 23. Mafunzo hayo yameanza leo Juni 14, 2022 mjini Iringa na yatahitimishwa hapo kesho Juni 15.

Maswali yatakayoulizwa katika sensa ya mwaka 2022.

  • Taarifa za Kidemgrafia, Umri, Jinsi, Uhusiano, hali ya ndoa na kadhalika
  • Maswali yanayohusu ulemavu.
  • Taarifa za uhamiaji.
  • Taarifa za Elimu.
  • Maswali kuhusu umiliki wa nyaraka za kitaifa ( Kitambulisho cha NIDA, Mzanzibar, mkazi cheti cha kuzaliwa, hati ya kusafiri, leseni ya udereva na cha ujasiriamali)
  • Shughuli za kiuchumi.
  • Umiliki wa ardhi na taarifa za TEHAMA.
  • Taarifa za uzazi na vifo.
  • Vifo vitokanavyo na uzazi.
  • Hali ya nyumba za kuishi na umiliki wa rasilimali mbalimbali.
  • Maswali ya kilimo na mifugo.
  • Mifuko ya hifadhi ya Jamii.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents