Burudani

Yammi amcharukia Nandy

Mwanamuziki wa Bongo-Fleva nchini Yammi ambaye anafanya kazi chini ya Lebo ya (African Princess) ameonesha kuchoka kusubiri kutoa kazi mpya na kuamua kumkumbusha Boss wake ambaye ni Nandy ageukie Upande wake.

Hayo yamekuja baada ya Nandy Kupost kwenye ukurasa wake wa Instagram mafanikio ya (Dah Remix) aliyowashirikisha wasanii wa Hip-hop Joh Makini, Rosaree, GNako, Khaligraph, Moni na Stamina huku akitaka kufanya remix na wasanii wa Singeli.

Yammi aliijibu Posti kwa kuandika “Kwa sasa inatosha sasa geukia Upande wangu”.

Ikumbukwe kuwa Yammi mwezi uliopita alitoa wimbo uitwao “Love Crazy” akiwa na wasanii Lexsil na Ziibeats.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents