HabariMichezo

Yanga faini Mil.5 kwa kupita mlango usio rasmi vs Simba

Klabu ya Yanga imetozwa faini ya Sh. 5,000,000 (milioni tano) kwa kosa la kuingia uwanjani kwa kupitia mlango usio rasmi kuelekea mchezo tajwa hapo juu kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa Novemba 5, 2023.

Adhabu hii ni kwa kuzingatia Kanuni ya 17:(21 & 60) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.

Klabu ya Simba imetozwa faini ya Sh. 1,000,000 (milioni moja) kwa kosa la wachezaji wake kuchelewa kutoka nje ya chumba cha kuvalia, jambo lililosababisha mchezo tajwa hapo juu kuchelewa kuanza kwa dakika nne (4) hivyo kuharibu programu za mrusha matangazo ya runinga (Azam TV) ambaye ni mdhamini mwenye haki za matangazo ya runinga Ligi Kuu ya NBC.

Adhabu hii ni kwa kuzingatia Kanuni ya 17:60 ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents