Habari

Yanga ndege tena mpaka Mbeya? Hakika upendo wa Rais Samia ni zaidi ya mahaba

Gumzo kubwa katika soka la Tanzania kwa sasa ni mafanikio ya klabu ya soka ya Yanga ambayo imerejea nchini usiku wa wa kuamkia leo ikitokea katika fainali ya pili ya Michuano ya Kombe la Shirikisho nchini Algeria dhidi ya USM Alger ambapo katika mchezo huo Yanga ilishinda 1-0 bila na kushindwa kutwaa ubingwa kutokana na faida ya goli la ugenini ambalo Ulger walipata katika mchezo wake wa awali jijini Dar Es Salaam.

Rais Dkt Samia amekuwa chachu mpya katika soka la Tanzania licha ya kuweka juhudi mbalimbali kama serikali katika kuhakikisha michezo inasonga mbele, lakini alichukua jitihada za zaida katika kutoa motisha kwa Yanga na Simba ambazo zote zalikuwa zinashiriki michuano ya CAF.

Hatau hii imetafsiriwa kama jitihada za ziada katika kusaidia soka la tanzania na kuamsha hisia ambazo zililala kwa wapenzi wa soka, wadau pamoja na wachezaji lakini pia jitihada hizi zimetafsiriwa kubadilisha mambo kadhaa kama yafuatayo.

MAMILIONI YA RAIS SAMIA

Watanzania kwa sasa wameamka zaidi katika michezo baada ya kuona mafaniko ya timu kadhaa kufika katika hatua za juu ambazo hazijawahi kufikiwa. Klabu ya Simba miaka ya karibuni imeshuhudiwa ikifika hatua ya nusu fainali ya klabu bingwa Afrika. Kwa upande wa Yanga imeweka rekodi yake mpya katika soka la Afrika baada ya kufika katika hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho kwa mara ya kwanza. Serikali ya Rais Samia katika muamko huo walikuja na kampeni mbalimbali kuongeza chachu katika michezo kitu ambacho kimeonekana wazi kwa Watanzania.

RAIS SAMIA ATOA NDEGE KWENDA ALGERIA

Klabu nyingi za Tanzania zinajikongoja kwenye uchumi wa kujiendesha na baadhi ya timu hizo zipo kwenye mchakato wa kwenda kwenye kujitegemea. Suala la Rais Dkt Samia kutoa ndege ni jambo ambalo limeamsha hisia mpya lakini pia ni taa ya kijani kwa timu zingine kuona zinafanya vizuri ili zinufaike na upepo huu mzuri kwani kuna wakati timu zinashindwa kusafiri kutokana na ufinyu wa bajeti.

RAIS SAMIA ATOA NDEGE KWA YANGA KWENDA MBEYA

Yanga leo watakutana na Dkt Samia Ikulu jijini Dar Es Salaam kabla ya safari yao ya kwenda Mbeya kwa ajili ya mechi ya ligi ya NBC dhidi ya Mbeya City. Katika umuhimu wa mambo yote mawil,i Rais Dkt.Samia kwa mara nyingine ametoa ndege kwa Yanga kwenda Mbeya na baada ya hapo itawasubiri kwa siku mbili kabla ya kurejea Dar Es Salaam.

WACHEZAJI NJE WAKOSHWA NA HAMASA YA SOKA LA TANZANIA

Diarra amekula Tsh Milioni 9.7 kutoka kwa Diamond Platnumz baada ya kuonyesha uwezo mkubwa katika mechi ya Yanga dhidi ya USM Alger. Diamond anasimama kama mdau wa soka ambaye anapenda mambo mazuri, matokeo chanya. Kumpa zawadi Diara ambaye sio Mtanzania kuna jenga motisha mpya kwa wachezaji wa nje kuona Tanzania ni sehemu sahihi kwao hivyo kuongeza juhudi zaidi lakini pia kuitangaza hamasa ya soka la Tanzania katika maifa yao.

Katika mtazamo wa kawaida unaweza kuona ni jinsi gani Rais Samia alivyokuwa na mapenzi ya dhati na soka la Tanzania, motisha aliyonayo Diamond leo ni zao la motisha ya Rais Samia, Wengi wanatamani kuona kesho njema ya Rais Samia ili kuona maendeleo zaidi ya michezo nchini. Kongole Rais Dkt Samia, haya sio mapenzi bali ni Mahaba kwa soka la Tanzania.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents