Michezo

Yanga walazimishwa sare na Polisi Tanzania

Goli la Pius Boswita dakika ya 90 linaipatia pointi moja Polisi Tanzania mbele ya Yanga SC kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.


FT : Polisi Tanzania 1 – 1 Yanga SC. Yanga imeruhusu bao hilo dakika za majeruhi kabisa wakati ambao baadhi ya mashabiki wengi wa #yangasc wakiamini mpira umekwisha na wanaondoka na alama tatu muhimu ili kujiimarisha zaidi kileleni.

Yanga imekuwa katika kipindi kisicho kizuri kwa matokeo ya hivi karibuni #vpl kwani kabla ya leo wiki iliyopita Wananchi walijikuta wakiacha pointi tatu muhimu pale Uwanja wa Mkwakwani baada ya kufungwa magoli 2 – 1 dhidi ya Coastal Union.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents