Michezo

Yanga wameingia mchecheto, wamekimbia mji – Ahmed Ally 

Tambo za Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally akizungumza na mashabiki wa timu hiyo jijini Mwanza kuelekea nusu fainali ya Azam Sports Federation Cup dhidi ya Yanga.

”Mchezo wetu wa tarehe 28/5/2022 wa nusu fainali ya Azam Sports Federation Cup dhidi ya Yanga, ndiyo mchezo tuliyoutolea macho kweli kweli. Kwanza tuna kwenda kumfunga mtani wetu lakini kama haitoshi tunakwenda kuchukua Ubingwa wa Kombe la Shirikisho la Azam Sports.”- Ahmed Ally

Ahmed Ally ameongeza ”Kwenye Kombe la Shirikisho la Azam huku tutatoana damu, nafasi bado ipo, nafasi ya kuchukua Ubingwa bado ni nyeupe na ipo wazi. Tayari wameshaanza kuingia mchecheto, wamekimbia mji hii ni ishara tosha kwamba pumzi ya moto inawahusu siku ya Jumamosi.”

Simba SC inatarajia kucheza mchezo huo wa nusu fainali dhidi ya Yanga SC siku ya Jumamosi ya tarehe 28 jijini Mwanza.

Imeandikwa na @fumo255

 

Related Articles

Back to top button