Michezo

Yanga waweka Historia Mpya Afrika

Droo ya upangaji wa hatua ya makundi kwa mashindano hayo yote mawili itachezeshwa Oktoba 7 huko Cairo, Misri. Yanga itakuwa katika chungu cha pili katika Ligi ya Mabingwa Afrika ambacho pia kina timu za Raja Casablanca, Pyramids na CR Belouizdad. .
Chungu cha kwanza kina Al Ahly, TP Mazembe, Esperance na Mamelodi Sundowns huku chungu cha tatu kikiwa na timu za Al Hilal, Orlando Pirates, Sagrada Esperanca na AS FAR wakati huo katika chungu cha nne kutakuwa na Maniema, Stade d’Abidjan, MC Alger na Djoliba. .
Kwa kuwekwa chungu cha pili, Yanga kuna uwezekano wa kupangwa katika kundi moja na timu tatu kutoka katika nchi zinazozungumza lugha ya Kiarabu.
Kutakuwa na vyungu vinne katika upangaji wa makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo timu moja katika kila chungu zitaunda kundi moja la mashindano hayo na timu zilizopo katika chungu kimoja haziwezi kukutana. .
Ifahamike kuwa hii ni mara ya kwanza katika historia ya mashindano ya klabu Afrika kwa Yanga kuwa katika chungu cha pili kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents