Michezo

Yanga yakimbiza 16 mfululizo Unbeaten

Mabingwa watetezi, Yanga wameendelea kunyatia ubingwa wa Ligi Kuu Bara baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Fountain Gate, huku ushindi huo uliofanya Yanga kufikisha pointi 70, umeweka rekodi ndani ya kikosi hicho.
.
Yanga imecheza mechi 16 mfululizo za msimu huu bila ya kupoteza, tangu mara ya mwisho kikosi hicho kilipochapwa mabao 3-1 dhidi ya Tabora United, Novemba 7, 2024. Katika michezo hiyo 16, Yanga imeshinda 15 huku mmoja pekee ukiisha kwa suluhu (0-0) ambao ulikuwa ni dhidi ya maafande wa JKT Tanzania.


.
Rekodi hiyo ya kucheza michezo 16 ya Ligi Kuu bila ya kupoteza, imeifikia pia ya Simba ambayo nayo imecheza idadi sawa ya mechi kama hizo, ambapo kikosi hicho tangu kichapwe na Yanga bao 1-0, Oktoba 19, 2024, hakijapoteza tena hadi leo. Katika michezo hiyo 16 ya Simba ambayo imecheza mfululizo ya Ligi Kuu bila ya kupoteza, imeshinda 14, huku miwili pekee dhidi ya Fountain Gate na Azam FC ikiisha sare.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents