Yanga yatua Sumbawanga

Kikosi cha Mabingwa wa Kihistoria wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga SC tayari kimewasili Sumbawanga kikiwa tayari kuwakabili Tanzania Prisons.

Yanga itashuka katika Uwanja wa Nelson Mandela majira ya saa 10:00 alasiri kuwakabili Tanzania Prisons kwenye mchezo huo wa hatua ya 16 bora ya Michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC).

Yanga italazimika kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo muhimu wa 16 bora ili kuongeza morali ya ushindi kwa wachezaji wake na mashabiki baada ya kushuhudia matokeo mabovu kwenye mechi yake ya mwisho walishuka dimbani ambayo ilikuwa Ligi Kuu wakipokea kipigo cha goli 1 – 0 kutoka kwa Matajiri wa jiji la Dar es Salaam, waoka mikate Azam FC.

Related Articles

Back to top button