Michezo

Yanga yavuna mkwanja mrefu balaa

Klabu ya Yanga baada ya kufanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali kwa kumfunga CR Belouizdad kwa idadi ya mabao 4-0 katika Uwanja wa Benjamini Mkapa wamejihakikishia USD $ 900,000 sawa na Tsh 2.3 Billion.

Yanga pia wamejiongezea alama 3 kwenye (CAF RANKING), hii inamaanisha Yanga watasonga mbele kutoka nafasi ya 18 waliopo na kuelekea juu zaidi.

Tofauti kati ya Yanga ya Nabi na hii ya Gamondi ni aina ya mpira unaochezwa sasa tofauti na ya kipindi cha nyuma huku kipindi hiki cha Gamondi ukatili ukiwa umezidi mara dufu.

Kutokana na takwimu za msimu uliopita  Yanga walishinda idadi ya magoli (4+) kwenye mechi moja tu katika michezo mitatu tu. Misimu huu wameshinda magoli (4+) kwenye mechi 1 katika michezo 9 mpaka hivi sasa;

Yanga dhidi ya KMC (5-0).

Yanga dhidi ya JKT Tanzania (5-0).

Yanga dhidi ya ASAS Djibouti (5-1).

Yanga dhidi ya Simba (5-1).

Yanga dhidi ya Mtibwa Sugar (4-1).

Yanga dhidi ya Jamhuri kutoka Zanzibar (5-0).

Yanga dhidi ya Housing Fc (5-1).

Yanga dhidi ya Polisi Tanzania (5-0).

Yanga dhidi ya CR Belouizdad (4-0).

Mpaka sasa kwa takwimu Yanga ya Gamondi ina uhatari zaidi ishakuwa tishio kwa vigogo Afrika, uwekezaji wa Yanga unazidi kuwalipa na hii inapandisha sana thamani Ligi ya Tanzania pale wawakilishi wetu kwenye klabu Bingwa Afrika wanapowatwanga vigogo.

Yanga wanatarajia kumaliza mchezo wao wa mwisho hatua ya makundi huko Cairo nchini Misri dhidi ya AL Ahly utakaopigwa mnamo tarehe 1 mwezi wa 3 siku ya Ijumaa major ya saa 1:00.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents