Michezo

Yao Yao aonyesha magumu anayopitia Yanga

Beki wa kulia wa Yanga, Yao Kouassi amesema maisha ya mchezaji wa mpira si ya mafanikio tu, pia kuna nyakati ngumu hukutana nazo.

Yao ameweka picha aliyofanyiwa upasuaji wa goti na kuweka ujumbe kuonesha ni namna gani anapitia maumivu kwa sasa.

Katika ujumbe huo amesema: “Tuwe na utamaduni wa kukubali kwamba si kila kitu katika maisha yetu kinapaswa kuwa chepesi au kizuri kila wakati.

“Kushinda kweli kunakuwepo na nyakati ngumu pia zina nafasi katika maisha yetu. Kila mtu anaweza kupitia changamoto yote ni suala la muda na kufanya kazi kimya kimya ili kurudi kileleni,”amesema beki huyo ambaye ana muda mrefu yupo nje ya uwanja kutokana na majeraha.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents