Michezo

Yaya Toure atua Liverpool, Son ajifunga miaka minne Tottenham

Mashabiki wa klabu ya Liverpool wamepata mshangao baada ya timu yao kuachia picha ambazo zinamuonesha mchezaji wa zamani wa Man City, Yaya Toure akiwa kwenye kambi ya mazoezi ya majogoo hao.

Toure ameoneka akiwa na baadhi ya nyota wa Liverpool ambao wapo kambini kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu.

Hata hivyo Toure alikuwa kambini hapo kama mgeni rasmi na rafiki wa karibu wa Sadio Mane ambaye amemualika kujionea namna Liverpool namna wanavyojiandaa na msimu.

Toure kwa sasa amejiunga na kozi ya ukocha akiwa na ndoto za kujakuwa Kocha mkubwa siku moja.

Akizunga na Liverpoolfc.com, Mane amesema ‘‘Nilipomuuliza Yaya kama anadhani ni wazo zuri kuja kuangalia mazoezi yetu, akanijibu, rafiki yangu ninakuja ila muulize kocha wako.”

”Yeye ni rafiki yangu mkubwa, mtu mzuri na  tumefahamiana tangu mwaka  2004..”

Na huko Tottenham, mchezaji nyota wa klabu hiyo Son Heung-min amesaini dili la miaka minne kuendelea kusalia kwenye timu hiyo.

Heung-Min Son: Tottenham forward signs new four-year deal until 2025 |  Football News | Sky Sports

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Tottenham Ijumaa hii Mkorea huyo ataendelea kusalia hapo npaka mwaka 2025.

Mshambuliaji huyo alijiunga na Tottenham akitokea Bayer Leverkusen mwaka 2015.

Son mwenye umri wa miaka 29, amefunga jumla ya magoli 107,  Assits 64 akiwa amecheza jumla michezo 280 ya mashindano yote ndani ya misimu yake sita Tottenham.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents