Yesu aonekana Ufaransa kwenye jengo la kanisa katoliki lililoteketea kwa moto, Wadau wapingana mitandaoni
Mwanamama Lesley Rowan amejikuta akizua gumzo kwenye mitandao ya kijamii duniani baada ya kuposti picha ya Jengo la kanisa la Notre Dame lilivyokuwa linaungua na kuonesha muonekano wa picha iliyozua sintofahamu.
Mwanadada huyo, amesema kuwa alivyoona picha za kanisa hilo likiungua yeye aliona picha ya ajabu kwenye moto huo ambayo aliamua ku-share kwenye ukurasa wake wa Facebook na kuomba maoni ya wadau kama nao wameona kitu alichokiona.
Maoni ya watu wengi walifananisha picha hiyo na picha ya Yesu ingawaje hakuna ushahidi wa kuaminika.
Kanisa la Notre Dame limeungua Jumatatu hii na ni moja ya makanisa maarufu barani Ulaya.
Tayari Rais wa Taifa hilo, Emmanuel Macron ameahidi kujenga upya kanisa hilo ndani ya miaka mitano.
Rais wa Marekani, Donald Trump naye ameahidi serikali yake kuchangia katika ujenzi wa Kanisa hilo lililojengwa karne ya 12.