Young Lunya na DJ Neptune wakomesha kwenye Great Ness IIl Albamu
Staa wa muziki na DJ maarufu kutoka Nchini Nigeria, DJ Neptune ameachia Albamu yake mpya iitwayo Great Ness III, ambayo amefanya kazi na mastaa wa kubwa wa muziki akiwepo Young Lunya kutoka Tanzania.
Albamu ya ‘Great Ness III’, ina ngoma zipatazo 14 na ngoma ya kwanza ambayo ina mahadhi ya Hip Hop ni Normal Day, ambayo Young Lunya na Khaligrap Jones kutoka Kenya wametisha. Mbali na mastaa hao wa Afrika Mashariki pia albamu hiyo ina wakali kama Qing Madi, Joeboy na Joshua Baraka kutoka Uganda na kwingineko.
DJ Neptune ameachia ngoma ya HONEST, leo ngoma ambayo amefanya na Qing Madi.
Great Ness I ilitoka 2018, Great Ness II ikatoka 2021 na sasa Great Ness III ipo tayari kwenye Digital Platform zote.
Watch HONEST feat. Qing Madi – https://youtu.be/yg785aHz79o