Habari

Zaidi ya watu 160 wafariki kwa mafuriko DRC

Maafisa wa Umoja wa Mataifa wanakadiria kwamba zaidi ya watu 160 wamekufa katika mafuriko mabaya zaidi yaliyoukumba mji mkuu,

 

Kinshasa, nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu OCHA imesema kufikia Disemba 16, mamlaka za Kongo ziliripoti kwamba angalau watu 169 wamekufa na wengine karibu 30 wamejeruhiwa na kupokea matibabu katika hospitali mbalimbali na angalau nyumba 280 ziliharibiwa.

Serikali haijatangaza ongezeko la idadi ya watu waliofariki tangu ofisi ya waziri mkuu ilipotaja idadi hiyo kuwa watu 120 siku ya Jumanne.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents