Burudani

ZaiiD ayakimbia ya Alikiba, Ommy Dimpoz na Ben Pol

Msanii wa muziki Bongo, ZaiiD amesema hakubadili rangi ya nywele zake katika video ya wimbo wake mpya ‘ Picha’ mara baada ya kuona wasanii wengine kama Alikiba, Ommy Dimpoz, Ben Pol na wengineo wakifanya hivyo..

ZaiiD amasema awali kuna wimbo wake unaitwa Ndanda Kosovo ndio alipanga ku-shoot video yake akiwa amebadili rangi ya nywele, hata hivyo alikuja kusitisha kutokana ulikuwa katika mahadhi ya trap na ukizingatia wimbo wake uliopita ulikuwa hivyo hivyo.

“Sasa tulipobadilisha tukaanza ku-shoot picha na script alizotumia Adam Juma zilikuwa zinamtaka mtu wa ofisini ambaye yupo rafu. Kwa hiyo mimi nikamwambia nina nywele za hivi akaniambia haina tatizo hivyo tukaendeleza,” ZaiiD ameiambia Bongo5.

Utakumbuka Alikiba alibadili rangi ya nywele zake katika video ya wimbo wake uitwao Mvumo wa Radi, Ommy Dimpoz alifanya hivyo katika wimbo wake ‘Yanje’, pia Ben Pol katika wimbo Tuliza Boli.

Related Articles

Back to top button