Zari awapiga STOP Wema na Aunty Ezekiel kwenda Afrika Kusini kwenye Birthday ya Tiffah ‘mtanichafulia nyumba yangu’

Mzazi mwezie na msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, Zari ameukataa ugeni wa mastaa wa filamu kutoka Tanzania Wema Sepetu na Aunty Ezekiel.

Related image
Zari

Marufuku hiyo ya Zari imekuja masaa machache baada ya Diamond kutangaza kuwa kwenye Birthday ya mtoto wao Tiffah kutakuwa na wanakamati 10 kutoka Tanzania ambapo kati ya hao yumo EX wake Wema Sepetu na Aunty Ezekiel kwenye sherehe ya 40 ya mtoto wa Mtangazaji wa runinga Zamaradi Mketema.

Zari kupitia mtandao wa Instagram amesema hataki ugeni wowote kutoka kwa watu hao kwani amedai atachafuliwa tu nyumba yake.

Sitaki kunichafulia nyumba yangu samahani naomba mkae huko huko“,amefunguka Zari baada ya kuulizwa swali na mmoja ya mdau kwenye mtandao wa Instagram.

Mapema mwezi huu Diamond aliahidi kupeleka mashabiki wake 30 nchini Afrika Kusini kusherehekea siku tatu Birthday ya Tiffah kuanzia tarehe 17 hadi 19 Agosti 2018.

Tiffah amezaliwa tarehe 06 Agosti na sherehe hiyo itakuwa ni ya kipekee soma zaidi kuhusu tukio hilo – Diamond Platnumz atangaza habari njema kwa mashabiki wa WCB.

Related Articles

36 Comments

Back to top button