Bongo5 Makala

Ziara ya rais ya acha alama isiyofutika Morogoro

Rais Samia Suluhu Hassan anahitimisha ziara yake ya kikazi ya siku sita katika Mkoa wa Morogoro, huku akiacha alama nne zitakazobaki kama kumbukumbu kwa wakazi wa mkoa huo.

Katika ziara hiyo iliyoanza Agost 2-7, mwaka huu Pamoja na mambo mengine mkuu huyo wa nchi alizindua Kampeni ya ‘Tutunzabe Mvomemero 2023-2028, ’Daraja la Berega lililopo na kuwapatanisha wakulima na wafugaji kwa kuwataka wapeane mikono kama ishara ya kumaliza migogoro ya wakulima na wafugaji, kusikiliza na kutatua migogoro ya kisheria kupitia Mama Samia Legal Aid Campaign.

Ziara hiyo iliambatana na wa Hospitali ya Wilaya ya Gairo na kuzungumza na wananchi katika mkutano uliofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi Gairo.

Sambamba na hayo, Rais Samia aliwasihi wawekezaji waendeleee kuwekeza kwenye teknolojia na mbinu za kisasa katika uzalishaji ili kupunguza gharama na kuongeza tija zaidi.

Mkuu wa nchi pia amewata viongozi kutumia kampeni mbalimbali za suluhisho la Amani badala ya kutoa matamko.

“Kilio kilichopo ni kwamba hawasimamii serikali za vijiji, watu wakishaumizana huko ni rahisi kunyoosha mkono kupokea kuliko kuleta suluhu,” anasema.

Aliwataka kuwasimamia wenyeviti wa vijiji waache kunyoosha mikono ,na walete suluhu za kweli nacsheria lazima zifuatwe.

Rais Samia pia alimtaka kila Mwananchi kuheshimu Uhuru wa mwenzake kwa kila shughuli anayoifanya ikiwemo ya kilimo na ufugaji kwani wote wanategemeana katika maisha ya kila siku.

Aliwataka wakuu wa wilaya na mikoa kuwachukulia hatua wale wote watakaoingilia uhuru wa watu kwa manufaa binafsi.

“Kila mmoja aheshimu mipaka ya mwenzie, kama unataka kulisha mifugo kalishe kwenye malisho sio kwenye mashamba, nanyie wakulima muncher kukata mifugo ya wenzenu” alisema.

Akizungumzia mradi wa Tutunzane Mvomero anasema kuna haja wafugaji kufanya ufugaji wa kisasa ikiwemo kuwa na maeneo yao ya kulima malisho ili kuondokana na migogoro kati yao na wakulima na watumiaji wengine wa ardhi kila uchao.

“Kampeni hii ni muhimu kwetu kwa sababu inakwenda kuleta amani, kuleta ongezeko la malisho, tija na wafugaji kuweza kukopesheka”, alisema Rais Samia.

Aliongeza kwa kusema kuwa mradi huu ukitunzwa vizuri uzalishaji wa sukari utafikia tani 550,000.

Wakati akizindua kampeni hiyo Rais Samia alisema mradi huo wa kuhamasisha ufugaji wa kisasa una umuhumu mkubwa kwa wafugaji na jamii inayowazunguka.

Akizungumza na wananchi hao, Rais Dkt. Samia aliwataka kuendelea kuzalisha zaidi mazao ya biashara na ya chakula.

Akizindua Daraja la Berega lililopo Wilayani Kilosa ambalo linaunganisha Wilaya hiyo na Wilaya ya Kilindi Mkoani Tanga, amewataka wananchi wa Kilosa kutunza miundombinu ya Daraja hilo ili liwe chachu ya uchumi kwao na kuwaletea maendeleo.

Aidha, Rais Samia alimtaka Waziri wa Kilimo kuangalia namna ya kuwasaidia wazalishaji wa zao la mbaazi kwa lengo la kuwawezesha kunufaika na bei bora zaidi.

Vilevile Dkt. Samia pia alizungumza na wananchi wa Dumila ambapo alisema kuwa Serikali inaendelea kuifanya kazi migogoro baina ya wakulima na wafugaji.

Bwawa hilo la Mtibwa la kutengenezwa lina uwezo wa kumebeba Lita bilioni 25.

Katika hatua nyingine,Rais Samia amezitaka mamlaka za mikoa na wilaya nchini kuhakikisha wanawasimamia vyema wenyeviti wa vijiji ili waache kupokea rushwa ili kuleta suluhu ya migogoro ya ardhi.

kuwapatanisha wakulima na wafugaji kwa kuwataka wapeane mikono kama ishara ya kumaliza migogoro ya wakulima na wafugaji.

“Maugomvi mwisho leo na kwamba sasa wote mnakwenda kubadilika na kuingia kwenye mradi mkabadilike mlime mnaolimanna mnaofuga mkafuge, hakuna haja ya kugombana, mtumie mradi huu ,nyie wote mnatupa uhai na mnatupa vitoweo na vyakula” alisema.

Aliongeza kwa kusema kuwa kampeni hiyo itasaidia pia kutunza mazingira na kuepusha athari zake huku akiwataka Wakulima na Wafugaji kuheshimiana kwa sababu wote wanategemeana.

Aidha, Rais Samia alitoa pongezi kwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi pamoja na serikali ya mkoa wa morogoro kwa ubunifu wao huku akiwaahidi kuwa Serikali yake itaendelea kuiunga mkono kampeni hiyo ya mfano hapa nchini.

Alifafanua kuwa sekta za mifugo na kilimo zimeajiri watu wengi nchini, na kwa sababu hiyo ataendelea kuweka msukumo ili kampeni hiyo iweze kuleta mabadiliko na mapinduzi makubwa kwa wafugaji na wakulima ili kuwainua na kuwanufaisha wananchi walio wengi.

Halikadhalika aliwaeleza wafugaji na wakulima kuwa mabadiliko hayaepukiki hivyo ni muhimu wakaunga mkono kampeni hiyo ili waweze kuepukana na migogoro ya kila uchao.

Beatrice Mpembo alisema wameambatana na Rais Samia ili kusikiliza na kutatua changamoto za wananchi wanaohitaji msaada wa kisheria.

“Tutakuwa na Rais muda wote wa ziara hapa Morogoro na tupo na Waziri wetu mheshimiwa Pindi Chana na wasaidizi wa kisheria ngazi ya wilaya na mkoa, kila anapofika mheshimiwa Rais kama kuna mtu anachangamoto ya kisheria tunaichukua na kuifanyia kazi,” alisema

“Kupitia ziara hii tumeshatoa msaada wa kisheria kwa wananchi mbalimbali na hata jamii ya wamasai tumekutana nao kwenye maeneo mbalimbali na tumewapa elimu ya sheria kuhusu migogoro yao ya mara kwa mara ya ardhi,” alisema Beatrice.

Alisema wakati wanasheria wengine wakiwa kwenye ziara hiyo, Rais Samia ametuma wanasheria wengine kupitia Kampeni ya Mama Samia Legail Aid kutoa huduma za msaada wa kisheria kwenye maonyesho ya nane nane mkoani humo.

Kwa upande wake, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, alimshukuru Rais Samia kwa maono yake na falsafa yake ya 4R ambayo ndio imepelekea kampeni hiyo kuanzishwa.

Vile vile Ulega alitoa shukrani za Wizara yake kwa uongozi wa mkoa na wiaya akisema “Rais, napenda pia kuwashukuru Mkuu wa Mkoa wa Morogoro na Mkuu wa Wilaya ya Mvomero kwa kuhamasisha Kampeni hii inayoakisi maono yako ya 4R – yaani Reconciliation (Maridhiano), Resilience (Ustahimilivu) Reform (Mabadiliko) na Rebuilding (Kujenga Upya), katika kuleta maridhiano baina ya jamii za wafugaji na wakulima”.

Waziri Ulega aliongeza kuwa Kampeni hiyo imefanikiwa kuhamasisha wafugaji na wakulima 825 kushiriki kwa vitendo katika kampeni hii.

“Jumla ya mashamba ya wafugaji 365 yamepimwa na kutengenezewa hati, na miundomibu ya maji kwa wafugaji imejengwa ikiwemo visima sita.
Vilevile, jumla ya tani 10 za mbegu za Juncao, kilo 462 za mbegu za Rhodes na miche 10,000 ya miti ya malisho aina ya Leucaena zimegaiwa kwa wananchi ambao ni wanufaika Kampeni hii.

Ziara hiyo Aliahidi kufanyia kazi ombi la ujenzi wa Barabara ya Wami-Dawawa-Madizini lililotolewa na kiwanda cha Mtibwa.
Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe alisema Serikali inatoa Sh220 bilioni ikiwa ni misamaha ya Kodi katika seta ya sukari.

Misamaha hiyo, alisema inalenga kuhakikisha sekta ya sukari nchini inaimarika, huku uzalishaji ukiongezeka.
Kwa mujibu wa Bashe, Serikali kwa sasa inaandaa Sera ya Taifa ya fedha katika sekta ya kilimo ili kuhamasisha uwekezaji wa muda mrefu.

Written by Janeth Jovin

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents