Afya

Zifahamu dalili za Omicron, aina mpya ya kirusi cha Corona

Aina mpya ya virusi vya corona vya Omicron vinaenea kwa kasi duniani kote. Je ni dalili gani watu wakipata wanapaswa kuchukua hatua?

Shirika la Afya Duniani (WHO) linasema watu bado wanapaswa kuangalia dalili za kawaida za Covid:

  • aina mpya ya kikohozi kinachoendelea
  • homa/joto la juu
  • kupoteza au kubadilika kwa harufu au ladha

Mpaka sasa kwa mujibu wa baadhi ya data za Uingreza, dalili tano za virusi vya corona vya Omicron ni hizi:

  • Mafua mepesi
  • kichwa kuuma
  • uchovu
  • kupiga chafya
  • kikohozi

Kama unadhani kuwa una corona, ni muhimu kufanya vipimo.

Hata watu ambao hawajisikii vizuri wanaweza kuwaweka wengine katika hatari ya kuumwa .Lakini watafiti wanasema , kuwa na uviko 19 kunaweza kukufanya mtu ujisikie kama una mafua makali au baridi.

Je nikipata homa, ina maana nina virusi vya corona?

Kiwango cha juu cha joto cha 37.8C au kuendelea.

Homa kama hii inaweza kuja wakati mwili ukiwa unapambana na maambukizi na sio virusi vya corona tu.

Graphic showing how to take your temperature using different types of thermometers

Ni bora kutumia kipima joto-thermometer. Lakini ikiwa huna, angalia ikiwa wewe, au mtu ambaye una wasiwasi naye, anahisi joto kwa kuguswa kwenye kifua au mgongo.

Joto kali hali na baridi hivi, Ikiwa una homa, panga kufanya vipimo vya coronavirus.

Vipi kuhusu kikohozi?

Ikiwa una homa au mafua unaweza kuwa na kikohozi, pamoja na dalili nyingine.

Mafua kwa kawaida huja ghafla na wagonjwa mara nyingi watapata maumivu ya misuli, baridi, maumivu ya kichwa, uchovu, koo kuwasha na mafua kutiririka au kujaa puani, pamoja na kikohozi. Unaweza kujihisi vibaya zaidi kuliko baridi kali.

Symptoms chart

Baridi ina mtindo wa kuanza taratibu na haina maumivu makali, ingawa inakufanya usijisikie vizuri pia.

Pamoja na kifua, labda na kupiga chafya, maumivu ya koo na mafua .

Covid-19: Tunachojua kuhusu Omicron na athari zake kwa Afrika

Homa, maumivu ya mwili na kichwa kuumwa huwa ni maumivu yanayotokea mara chache.

Kikohozi cha virusi vya corona, huwa kinakufanya mtu ukohoe sana zaidi ya saa, saa tatu au zaidi ndani ya saa 24.

Kama huwa unakohoa kwa sababu unapata matibabu ya hali ya kiafya ya muda mrefu, basi kikohozi kitaongezeka na hali kuwa mbaya zaidi.

Unapaswa kupima virusi vya corona kama umeanza kukohoa kwa mfululizo.

Kupoteza au kubadilika kwa harufu au ladha kunamaanisha nini?

Hii ni dalili kuu za coronavirus na inamaanisha unapaswa kupimwa.

Bado inaweza kuwa una mafua tu, wakati wa baridi. Lakini unahitaji kuangalia, hata kama hujisikii vizuri, ili kuepuka hatari ya kueneza virusi.

Je, kupiga chafya kunamaanisha kuwa nina virusi vya corona?

woman blowing her nose

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Kupiga chafya sio dalili ya kawaida ya coronavirus. Matone ya kupiga chafya yanaweza kueneza maambukizi ingawa, hivyo ni muhimu kunawa mikono yako au kutumia tishu.

Ili kusaidia kuzuia kuenea kwa coronavirus na magonjwa mengine:

• Nawa mikono mara kwa mara

• Vaa barakoa katika mkusanyiko wa watu

• Jaribu kuwa mbali na wale ambao hawakai nyumbani kwako.

Vipi kuhusu mafua kutiririka au pua kuziba au maumivu ya kichwa?

Mamlaka ya afya yanasema kuwa na mafua au maumivu ya kichwa sio dalili za Covid.

Lakini utafiti unasema baadhi ya watu wanaopima na kukutwa na Covid wana dalili hizi.

Muongozo wa Marekani unaangazia dalili zifuatao kujua kama mtu ana uviko:

  • Homa
  • Kikohozi
  • Kupumua kwa shida
  • Kuhisi uchovu
  • Maumivu ya mwili na misuli
  • Maumivu ya kichwa
  • Kupoteza ladha au kubadilika kwa harufu
  • Koo kuwasha
  • Mafua
  • Kutapika
  • Kuharisha

Je kama sijisikii vizuri?

Watu walio na virusi vya corona wana dalili mbalimbali, kuanzia dalili kidogo hadi kali. Baadhi hawatakuwa nayo kabisa, lakini bado wanaweza kuambukiza.

Dalili zinaweza kuonekana hadi wiki mbili baada ya kuathiriwa na coronavirus, lakini kawaida karibu siku ya tano.

Kuhisi kukosa pumzi kunaweza kuwa ishara ya maambukizo makubwa zaidi ya coronavirus.

Ikiwa unapata shida ya kupumua, wasiliana na daktari wako mtandaoni au kupitia simu.

Ikiwa una wasiwasi sana juu ya upungufu wa pumzi ghafla, piga simu uletewe gari la wagonjwa.

Pata ushauri wa daktari kama :

  • Una wasiwasi kuhusu mtoto mwenye umri wa chini ya miaka mitano
  • Mtoto wako hajisikii vizuri ,tafuta ushauri wa daktari.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents