Burudani

Zuchu ana nidhamu sana – Alikiba

 

Moja kati ya changamoto kwa wasanii wengi ni nidhamu. Ni kitu ambacho kimetajwa kuwakwamisha wasanii wengi wasifanikiwe licha ya kuwa na vipaji vya hali ya juu.

Mkali wa kuimba na mwenye tungo za kipekee ambaye pia ni Rais wa @kingsmusicrecords , @officialalikiba amefunguka kukoshwa na nidhamu ya msanii @officialzuchu kutoka lebo ya WCB ambayo inasimamiwa na @diamondplatnumz .

“Namba yangu hana nina uhakika, mimi pia namba yake sina lakini ni Msanìi ambaye napenda kazi zake anaimba vizuri na nilikutananaye Airport tukasalimiana, nilivyomuona tu She is very discolined ( ana nidhamu sana),” alisema Alikiba kupitia Clouds Fm.

Mashabiki wengi wa muziki wamependezwa na kauli hiyo ya ‘Kings’ kwa kuwa moja ya changamoto kubwa kwa wasanii wanaopata mafaniko mapema ni nidhamu.

Written and edited by @yasiningitu

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents