Bongo5 ExclusivesBurudaniHabari

Zuchu awakimbiza wakongwe wa muziki Africa, aongoza kwa Subscriber Youtube kwa wasanii wa kike

Hii ni kubwa sana kwenye muziki wetu wa Bongo Fleva baada ya kuona wasanii wa muziki wetu wanafanya vizuri kwenye baadhi ya sehemu hasa kwenye mtandao wa YouTube.

Diamond ndio msanii anayeongoza kwa subscriber Youtube kwa wasanii wa kusini mwa ajangwa la Sahara kwa wasanii wote wa kiume na wa kike lakini kwa wasanii wa kike Zuchu kutoka WCB ndio anaongoza kwa sasa.

Mwimbaji huyo wa Bongofleva toka WCB Wasafi, ameweka historia ya kuwa msanii wa kike katika nchi zilizopo chini ya Jangwa la Sahara barani Afrika kuwa na subscribers wengi katika mtandao wa YouTube.

Zuchu ambaye alitoka kimuziki miaka miwili iliyopita, amefikisha subscribers Millioni 2.1, nafasi ambayo amempiku msanii toka Nigeria, Yemi Alade mwenye subscribers Millioni 2 ambaye alikuwa anashikilia.

Kweye top 10 ya orodha hiyo, nafasi ya kwanza ni Zuchu, kisha anafuata Yemi Alade huku nafasi ya sita ikishikiliwa na Mtanzania, mwimbaji Nandy akiwa na subscribers Millioni 1.7

Tazama Orodha Ya Wasanii Wakike Kutoka Kusini Mwa Jangwa La Sahara (Africa) Wenye Subscribers (Wafuasi) Wengi Zaidi Katika Mtandao Wa Youtube.

1. @officialzuchu πŸ‡ΉπŸ‡Ώ – 2.1M
2. @yemialade πŸ‡³πŸ‡¬ – 2M
3. @therealsinach πŸ‡³πŸ‡¬ – 1.9M
4. @adaehimoses πŸ‡³πŸ‡¬ – 1.4M
5. @tiwasavage πŸ‡³πŸ‡¬ – 1.12M
6. @officialnandy πŸ‡ΉπŸ‡Ώ – 1.07M
7. @symplysimi πŸ‡³πŸ‡¬ – 853K
8. @diana_marua πŸ‡°πŸ‡ͺ – 756K
9. @chidinmaekile πŸ‡³πŸ‡¬ – 667K
10. @tenientertainer πŸ‡³πŸ‡¬ – 592K

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents