Burudani

Zuchu awavaa TCRA, awaandikia barua ya wazi

Baada ya siku ya jana Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania @TCRA_Tz KuIfungia video ya wimbo wa Diamond Platnumz na Zuchu unaoitwa “Watasubiri sana’ baada ya kupata taarifa kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kuwa wimbo na video hiyo inaleta ukakasi kwa waumini wa dini na dhehebu fulani.
Kupitia Instagram yake Zuchu ameandika haya:
“BARUA YA WAZI KWA BASATA NA TCRA
Ni matumanini yangu mpaka sasa kila mtu anafahamu kua Video Ya wimbo wetu pendwa “MTASUBIRI “ Umesitishwa kuonekana kwenye vyombo vya habari Nchini kwetu .Nimeona bora nianze moja kwa moja kwenye mada husika .
Jana Nilipokea taarifa hizi kupitia mitandao kama Nyinyi tu mashabiki zetu kwamba wimbo wetu unapigwa marufuku sababu tajwa kua inaleta ukakasi kwenye jamii husika mwisho wa kununukuu .
Awali ya yote niseme kama msanii nilietumia ubunifu kukaa chini na muongozaji wa video yetu takribani siku 4 kuunda stori ambayo kwa utashi wangu na heshima niliyonayo kwa dini zote na madhehebu yake sikuona huu ukakasi unaoongelewa hapa.
Nafahamu si kila kazi ya kisanaa itamfurahisha kila mtu lakini kuvunjia heshima dini si kitu ambacho kipo ndani ya weledi wa kazi yetu sababu tunafahamu fika tunao mashabiki wa dini zote na kulinda hisia zao ni moja ya nguzo kuu Kwenye mziki hatueki matabaka .Ifahamike kwamba mimi ndie nilishoot hiyo scene ikinataka kuwepo kanisani nikiwa nafanya mazoezi ya kwaya sio misa ni mazoezi ya kikwaya nikiwa nimevalia joho lenye stara .
Kanisa hili lipo kisarawe na kabla ya kushoot masister walitukagua na kusikiliza kwa makini stori yetu na kuridhishwa nayo ndipo hapo tukapewa ruhusa ya kushoot .Naomba nielekeze malalamiko yangu kwa mamlaka husika BASATA walezi na wazazi nimeambatanisha video na movie baadhi ambazo zimetoka kabla ya mtasubiri vipi hizi hazina ukakasi .Lakini ni jamii ipi hiyo iliyoleta malalamiko mpaka nyie kufungia video iliyogharimu muda wa siku nne na pesa nyingi kuishoot tena mkaifungia bila hata kutaka kusikiliza utetezi .
Mtasubiri video ni ya kawaida sana A very innocent sweet story .
Naumia sababu hii inaenda kudumaza sio tu mziki ila Tasnia nzima kwa ujumla .HAYATI baba wa taifa alisema “Utii ukizidi huzaa uoga ,Uoga huzaa unafiki na kujipendekeza mwisho wake Umauti “
Huu ndio umauti wa Tasnia hii unapoanzia
INAENDELEAA “

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents