FahamuHabari

Zuchu namba moja Afrika kwa wasanii wa kike wenye Subscriber wengi Youtube

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva kutoka katika lebo ya WCB Wasafi chini ya Naseeb Abdul alimaarufu Diamond Platnumz Zuhuru Othmani Zuchu amekuwa msanii namba katika bara la Afrika kwa wasanii w akusini mwa Jangwa la Sahara kwa kuwa na wafuasi (Subscribers) wengi katika mtandao wa Youtube.

Kabla ya @officialzuchu kushika namba moja Youtube kwa wasanii wa kike nafasi hiyo alikuwa anaishikilia msanii kutoka Nigeria Yemi Eberechi Alade.

Kasi ya Zuchu ni kubwa sana na ikumbukwe ni msanii ambaye hajamaliza hata miaka minne baada ya kutambulishwa rasmi WCB na kufungua mitandao yake mfano Youtube ukilinganisha na wasanii wakongwe kama Yemi Alade, Tiwa Savage na wengine.

Zuchu aliifungua akaunti yake ya Youtube rasmi Jan 29, 2019 huku Yemi Alade akifungua Nov 15, 2012.

Hii hapa ndio Orodha ya wasanii wanaoongoza kwa Subscribers katika mtandao wa Youtube.

@officialzuchu -2.29M
@yemialade -2.10M
@therealsinach -1.97M
@adaehimoses -1.147M
@tiwasavage -1.14M
@officialnandy -1.11M
@symplysimi -0.87M
@diana_marua 0.78M

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents