Bongo5 ExclusivesBurudaniDiamond PlatnumzMuziki

Zuchu ndio Malkia wa Bongo Fleva, Huu ndio wakati wake Album itaeleza(Video)

Inawezekana unampenda au humpendi, unamkubali au humkubali hilo haliwezi kuzuia ukali wake, ukweli ni kwamba Zuhuru Othman Soud alimaarufu @officialzuchu ndio msanii bora kwa sasa kwa upande wa wasanii wa kike sio tu Tanzania bali Afrika Mashariki nzima.

Achana na tuzo aliyochukua ya TMA mwaka huu kwamba msanii bora wa Bongo Fleva kwa mwaka 2023, kazi zake zinaeleza.

Ndio msanii pekee Afrika Mashariki mwenye uwezo wa kutengeneza Numbers nyingi kwenye mitandao ya Nyimbo (Music Platforms) kwa muendelezo wa miaka zaidi ya miwili mpaka sasa.

Ndio msanii pekee Afrika Mashariki mwenye wimbo una Viewers wengi Youtube zaidi ya milioni 100 wa Sukari ambao una miaka mitatu tu.

Ndio msanii pekee Afrika nzima mwenye Subscribers wengi kwenye akaunti ya Youtube kwa upande wa wasanii wa kike Afrika nzima.

Tanzania ndio msanii pekee aliyepanda majukwaa makubwa kwa mwaka 2023 kwa upande wa wasanii wa kike, alitumbuiza TRACE RWANDA 2023, alitumbuiza Jukwaa moja na Kendrick Lamar kwenye Tamasha la Inaugural Move Africa Festival 2023.

Ametumbuiza Marekani, Mayotte na mataifa mengine kwa miaka karibia miwili mfululizo kuanzia mwaka 2022.

Mambo hayo yanatosha kueleza kuwa @officialzuchu ndio msanii bora kwa sasa na ana future nzuri sana kwenye kiwanda cha Bongo Fleva hapo mbeleni.

Achana na kuwa kwenye lebel ya @wcb_wasafi bali angalia juhudi za msanii husika maana ukihusisha lebel pia kuna wasanii kadhaa kwenye lebel hiyo na amewapita mengi.

Inawezekana bado hajaanza kuimbwa kama akina Lady Jay Dee, Ray C, Vanneda Mdee na wengine lakini yupo kwenye njia sahihi ya kuelekea kule.

Mpaka sasa ana miaka minne tu kwenye Game amefanya mengi na anaendelea kufanya mengi.

Hii itakuwa album yake ya kwanza kwenye maisha yake baada ya EP yake ya I AM ZUCHU iliyotoka wakati anatambulishwa WCB.

Alibum hii ndio itakuja kutoa mwanga muelekeo sahihi wa @officialzuchu Kimatifa ambapo anaweza kuingia kwenye ushindani na wasanii wenzake wa kike kama Tyla, Ayra Starr, Tems na wengine.

Uansishi wake ndio unawavutia wengi, amekuwa na muendelezo mzuri wa kuandika nyimbo zenye uwezo wa kuteka kila rika, amekuwa na ushawishi mkubwa.

Bonyeza link kuangalia video kamili

https://www.instagram.com/reel/DCWTWnGKdzM/?utm_source=ig_web_copy_link&igsh=MzRlODBiNWFlZA==

 

Imeandikwa na @el_mando_tz

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents