Michezo

Je yaliyomkuta Casemiro ndio mwisho wake??

AMIE Carragher amemtolea uvivu Casemiro na kumwambia muda wake umekwisha, afungashe virago akampumzike baada ya kucheza ovyo kwenye mechi iliyowashuhudia Manchester United wakikubali kichapo cha mabao 4-0 kutoka kwa Crystal Palace kwenye Ligi Kuu England usiku wa juzi Jumatatu.

Kilikuwa kiwango cha ovyo sana kutoka kwa Man United, lakini gwiji wa zamani wa Liverpool na Ligi Kuu England, Carragher amemwonyeshea kidole Casemiro na kudai shida ilianzia kwake. Hakika, Casemiro atakuwa na usiku wa kumbukumbu mbaya kwenye mechi hiyo baada ya kulambwa chenga na Michael Olise wakati anakwenda kufunga bao la kwanza, huku Mbrazili huyo alibaki akigalagala ardhini.

Kwa jumla, Casemiro alipitwa mara nane katika mechi hiyo, kitu ambacho kinaweka rekodi kwa mchezaji wa Ligi Kuu England kupitwa mara nyingi kwenye mchezo mmoja. Baada ya mechi hiyo, Carragher alisema sasa umefika wakati wa Casemiro kukubali yaishe na kuachana na soka, akisema kitu ambacho kiungo huyo anapaswa kufanya kwa sasa ni kuhamia tu kwenye ligi ya Marekani (MLS) au Saudi Pro League huko Saudi Arabia, kwa sababu amechoka. Carragher alisema:

“Nilisema wakati wa mapumziko, Ten Hag anapaswa kumtoa Casemiro. Najua alikuwa na watoto wadogo kwenye benchi, lakini nadhani Casemiro, amekuwa ovyo sana, alipaswa afahamu yeye ni mchezaji mwenye uzoefu na ajue tu, amebakiza mechi tatu za kucheza kwenye ushindani mkubwa. Mbili za ligi na moja ya fainali ya Kombe la FA.“

“Baada ya hapo, anapaswa tu kujua, anatakiwa kwenda MLS au Saudia. Niko siriazi. Amezeeka, watu wanayemzunguka, wanapaswa kumwaambia aachane na soka. Aachane na soka kabla ya soka halijamwaacha.”
Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents