Burudani

Miaka 20 ya Mmiliki wa Samaki Samaki

Miaka 20 ya Mmiliki wa Samaki Samaki, Kalito Tanzania, Aendelea Kuitangaza Kimataifa

Safari ya miaka 20 ya muwekezaji mbunifu Carlos Bastos,maarufu kama Kalito ambaye anamiliki migahawa ya Wavuvi Kempu, Kuku Kuku, Samaki Samaki,. Kalito ni raia wa Hispania aliyepata utambulisho kupitia rafiki kuhusu Tanzania. Alivutiwa na hadithi za uzuri wa asili na utamaduni wenye vionjo uliomo nchini.


Alifanya safari ya kuja Afrika Mashariki mwaka 2002, alipowasili aliona uzuri wa ardhi iliyojaa uhuru na furaha, tofauti kabisa na maisha ya Ulaya yaliyokuwa na ugumu kidogo. Alivutiwa zaidi na uzuri wa Tanzania, Kalito alifanya uamuzi wa kubadilisha maisha mwaka 2004 na kuhamia kabisa, kuweka msingi wa safari ya ujasiriamali.

Anaposherehekea miaka 20 nchini Tanzania, Kalito alimpongeza Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, pamoja na Marais wote waliopita, kwa kazi nzuri wanayofanya kuendeleza taifa. “Nawapongeza serikali zote ambazo nimeziona madarakani; wanajitahidi na kufanya kazi kwa bidii,” alisema Kalito.

Vilevile akiipongeza Serikali kwa kushirikiana nayo katika kuleta maendeleo nchini, Kalito ameeleza kuwa kutokana na maono ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, ya kutaka kuipeleka Coco Beach kimataifa, akiwa moja ya mnufaika wa sehemu hiyo aliamua kuleta party ya HELLO JUA ikiwa na maana ya kusherehekea siku mpya pale jua linapochomoza lakini kwa kuiboresha na kuifanya kimataifa.

“Tulipokuwa tunakabidhiwa Coco Beach tuliambiwa kuwa maono ya eneo hili ni kulifanya kuwa kivutio kwa watalii mbalimbali na kuifanya ifahamike kimataifa zaidi. Kutokana na biashara yangu ya burudani, nikaja na wazo la HELLO JUA party tufanye mara moja kwa mwezi kila siku asubuhi kusherehekea siku mpya,” ameeleza Kalito

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents