Burudani

Rapper Big Sean aanza kufuata nyayo za Diamond Platnumz

Rapper Big Sean kutoka Marekani ambaye pia anafanya kazi chini ya Lebo ya muziki ya G.O.O.D Music ya mnyamwezi Kanye West ameahidi kuanza kubadilisha staili yake ya kurap na kuanza kuimba.

Image result for big sean
Big Sean

Kwenye mahojiano yake na Jarida la Vibe, Big Sean amesema kuwa anajiona mtu mwenye sauti nzuri na hata watu wake wa karibu wamekuwa wakimwambia na tayari ameanza kuandika nyimbo.

Hata hivyo, mashabiki wake wengi wamebeza maamuzi hayo kwa kumtaka abaki kwenye staili ya ku-rap au afanye vyote kwa pamoja.

Maamuzi ya Big Sean yanaendana kabisa na ya Msanii wa Muziki hapa Tanzania, Diamond Platnumz ambaye naye miaka ya nyuma kabla ya kujulikana zaidi kwenye kuimba, alikuwa ni rapper na alishawahi kufanya kazi kadhaa ikiwemo Jisachi lakini baadae akaamua kuachana na muziki huo.

SOMA ZAIDI – Wengi hawajui, Diamond ni rapper – Producer Hermy B

Je, unadhani Big Sean huenda akafanya vizuri kwenye kuimba kuliko kwenye muziki wa Hip Hop? ikumbukwe kuwa mkali huyo mpaka sasa ameshatwaa tuzo kubwa kibao za muziki duniani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents