Habari

Samia Scholarship yafadhili Wanafunzi 1220

Serikali imeendelea kuimarisha fursa za upatikanaji wa elimu ya juu kupitia utoaji wa mikopo kwa Wanafunzi wa elimu ya juu ambapo imetoa ufadhili kwa Wanafunzi 1,220 kati ya 1,200 waliolengwa (Wanafunzi wapya 915 na wanaoendelea 305) wenye jumla ya Tsh. 6,367,169,632.00 kupitia SAMIA Scholarship.

Akiwasilisha Bungeni Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa Mwaka 2024/2024, Prof. Mkenda amesema Serikali pia imetoa mikopo kwa Wanafunzi 229,652 (mwaka wa kwanza 83,640 na wanaoendelea 146,012) yenye jumla ya Shilingi 786,724,730,000.00”

“Serikali pia imetoa mikopo kwa Wanafunzi 2,299 wa ngazi ya stashahada yenye jumla ya Shilingi 6,114,790,500.00 na imekusanya jumla ya Shilingi 132,731,358,063.47 sawa na asilima 55 ya lengo la kukusanya Shilingi bilioni 241 kutokana na mikopo iliyoiva”

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

cc:Millard ayo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents