Michezo

Sanaa ina mchango mdogo ukuaji wa pato la Taifa

Waziri wa Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo amesema mwaka 2023, sekta ya sanaa na burudani iliongoza kwa kuwa na ukuaji wa asilimia 17.7 kifuatiwa na sekta ya fedha na bima asilimia 12.2, madini asilimia 11.3, malazi na huduma za chakula asilimia 8.3 pamoja na habari na mawasiliano asilimia 7.6

Akitoa hotuba ya hali ya uchumi wa Taifa kwa mwaka 2023, Bungeni Jijini Dodoma leo June 13,2024, Mkumbo amesema “Licha ya kuwa na ukuaji mkubwa, shughuli za sanaa na burudani zilikuwa na mchango mdogo katika ukuaji wa Pato la Taifa, hii imetokana na kuwa sekta hii imeajiriri Watu wachache wanaojishughulisha na kazi mbalimbali za sanaa ikilinganishwa na shughuli nyingine za uchumi, kazi hizo ni pamoja na maigizo, tamthilia, muziki, uchongaji, uchoraji, na ushonaji”

“Aidha, shughuli za kilimo, madini, ujenzi na fedha na bima zimeendelea kuwa kichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi kutokana na shughuli hizo kuwa na pato kubwa na kuhusisha sehemu kubwa ya jamii mijini na vijijini”

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents