Michezo

Simba wafanya umafia tena

Kule Zambia, bosi wa Simba Crescentius Magori ameshaimsainisha winga kiberenge Joshua Mutale kutoka Power Dynamos ya huko lakini akawaita chemba wachezaji wawili, akianza na kiungo mkanajo Kelvin Kapumbu kisha baadaye beki wa kati Tandi Mwape .
Zesco ya Zambia, ilikuwa inapambana kuwaongezea mikataba Mwape na Kapumbu, ili kutengeneza ukuta imara kwa ajili ya msimu ujao itakaposhiriki mashindano sawa na Simba ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Zesco inacholia ni kwamba mastaa hao wawili wa timu ya taifa ya Zambia wamekuwa wasumbufu ghafla kuendelea na mazungumzo wote wakitajwa kutiwa kiburi na Simba kupitia mazungumzo na Magori. .
“Kapumbu amekuwa hataki kupokea simu, tunataka kumuongezea mkataba, huku pia Tandi (Mwape) naye tulikuwa tunakwenda naye vizuri lakini amekuwa hajibu tena simu zetu na wote wawili walionekana na kiongozi wa Simba alipokuja hapa,” alisema bosi wa juu wa Zesco ambao ni Mabingwa wa zamani wa Soka nchini humo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents