Michezo

Story nzima ya Aubin Kramo na Simba

Simba inafikiria kuhamisha mechi zake za nyumbani kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha lakini winga Aubin Kramo anarudi uwanjani.

Habari za uhakika zinasema kwamba Kramo ameshakuwa fiti na sasa anajinoa na klabu yake ya zamani ASEC Mimosas tayari kwa msimu mpya na Simba baada ya kushindwa kufanya hivyo kutokana na majeruhi ya muda mrefu.

Staa huyo alikuwa anapewa nafasi kubwa kutemwa na Simba lakini Habari za ndani ni kwamba wamejiridhisha kwa vipimo vya kitabibu kwamba msimu ujao anaweza kukiwasha Msimbazi na akarejea kwenye rekodi zake.

image

 

Lakini habari za ndani ambazo Mwanaspoti imezipata ni kwamba Simba wanafikiria kuhamishia mechi zao za nyumbani msimu ujao kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha.

Habari zinasema asilimia kubwa ya uongozi wanalijadili hilo, na kwamba Dar es Salaam wamepanga kuchezea mechi zao za Kombe la shirikisho tu.

Za ndani zinasema kwamba wanaona kama Dar es Salaam pamekuwa pagumu kwao katika misimu ya hivi karibuni kwani kumekuwa na mambo mengi.

 

Simba wanaamini kwamba pia Arusha kuna mashabiki wao wengi na hata miundombinu ya viwanja vya mazoezi na kambi ni rafiki.

 

 

Ingawa lolote linaweza kutokea watakaporudi kwenye kambi ya mazoezi nje ya nchi, lakini mpaka sasa wameanza kuwasiliana na mamlaka za Arusha kuona jinsi ya kuuboresha uwanja wa Arusha.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents