Habari

Waislamu walazimishwa kula kitimoto na kunywa pombe nchini China, mamlaka zatoa vitisho kwa watakaokaidi

Waislamu mjini Xinjiang nchini China walilazimishwa kula nyama ya nguruwe na kutumia vileo kwenye sherehe za mwaka mpya wa jadi wa China.

Passengers ride a donkey cart at the venue for a Chinese Lunar New Year shopping festival in Lopnur county, Bayingolin Mongol Autonomous Prefecture in Xinjiang

Kwa ushuhuda uliotolewa na wakazi wa Ili Kazakh mjini Xinjiang, wamesema kuwa siku ya kilele cha siku hiyo, walialikwa kama desturi ya Wachina wanaposherehekea na kuamliwa kula kitimoto na kunywa pombe.

Kwa mujibu wa kituo cha Radio Free Asia, kimeripoti kuwa mamlaka za mji huo unaokaliwa na takribani waislamu milioni 10, ziliwataka waislamu kusherehekea kwa nguvu sherehe hizo, ambazo zinapingana na imani ya dini ya Kiislamu .

Kituo hicho cha Radio, kimeripoti kuwa Mamlaka zilipitia kila nyumba na kuwataka washerehekee kwa kula na kunywa pombe, la sivyo watachukuliwa hatua kali ikiwemo kutupwa jela.

Uighur vendors trade Halal meat to costumers in the Tianshan District of Urumqi, capital of north-west China's Xinjiang region. Residents in the Ili Kazakh Autonomous Prefecture said they were invited to Chinese New Year dinners where pork and alcohol were served

Picha zilizosambazwa na kituo hicho cha Radio Free Asia, zinaonesha mamlaka za usalama mjini Yining zikigawa nyama ya kitimoto kwenye makazi ya waislamu siku ya Jumatatu Februari 4, huku zikiwataka wapambe nyumba zao kwa maua mekundu kama ishara ya kusherehekea mwaka mpya wa China.

A halal restaurant in Xinjiang. Both pork and alcohol are forbidden in Islam, and Chinese New Year is not usually celebrated by Muslims

Pombe na nyama ya kitimoto ni vitu ambavyo haviruhusiwi kutumiwa na Waislamu, na ndio maana ya Waislamu nchini China wanapinga kusherehekea sikukuu hiyo, ambayo ni kubwa na ni maarufu zaidi nchini humo kama ilivyokuwa sikukuu ya Kristmasi kwa Wakristo.

Watu wa Khazan, hawajawahi kula kitimoto, hata mwaka jana tulitishiwa na baadhi yetu walichukuliwa na polisi kwa kugoma kusherehekea sikukuu ya mwaka wa China. Sisi hapa tunajua sikukuu zetu ni Eid al-Fitr na Eid al-Adha hizo nyingine hatuwezi kusherehekea hata kwa nguvu,“amesema mkazi wa Khazan mjini Xinjiang .

SOMA ZAIDI – Historia ya sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China .

Serikali ya China katika Jimbo hilo, imekuwa ikitoa masharti magumu kwa waislamu wanaoishi jimbo hilo.

Mwaka 2017, Serikali ilipiga marufuku wanaume Waislamu kufuga ndevu ndefu na wanawake kuvaa hijab mjini Xinjiang linalokaliwa na Waislamu milioni 10.


Mwaka 2015, China ilizuia Waislamu wa Xinjiang kutofunga mwezi wa Ramadhan kwa kuhofia nguvu kazi ya taifa kupungua.

Chanzo: https://www.dailymail.co.uk/news/article-6682005/Muslims-China-forced-eat-pork-drink-alcohol-Lunar-New-Year-dinners.html

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents