Burudani
Rick Ross avunja ukimya baada ya kutoka hospitalini
Big Boss wa Maybach Music Group, Rick Ross amevunja ukimya kwa kuamua kutoa kauli yake ya kwanza baada ya kutoka Hospitali.
Rick ambaye alikuwa amelazwa katika hospitali moja mjini Florida baada kupata tatizo la kushindwa kupumua na kupoteza fahamu kutokana na nimonia amerudi mtaani rasmi na kuamua kuwajuza mashabiki zake katika mtandao wa kijamii wa Instagram.
https://www.instagram.com/p/BgD9x85l3mX/?utm_source=ig_embed
“Ain’t nothing like home 🙏🏼. I love y’all – WLR,” ameandika Rick Ross. Huku akiwa ameweka picha ya mtu aliyevaa koti lililoandikwa “Black Bottle Boys” mgongoni mwake na kushika chupa ya mvinyo ya Luc Belaire.