Burudani

Bondia maarufu Marekani achukizwa na watangazaji wa TMZ ‘Kanye West alistahili kipigo’

Mwanamasumbwi wa ngumi za kulipwa (UFC), Tyron Woodley amechukizwa na kitendo cha waandishi wa habari wa mtandao wa TMZ cha kumuacha salama rapa Kanye West baada ya kutoa kauli ya mauzi ya kusema kuwa “watu weusi walichagua kuwa watumwa kwa miaka 400“.

Tokeo la picha la tyron Woodley vs kanye west
Kanye West

Tyron amesema kauli hiyo haikuwa nzuri hususani kwa jamii ya watu weusi na mbaya zaidi Kanye alimsogelea mtangazaji, Van Lathan akitaka kupigana naye.

Sikuwa najua kilichoendelea baada ya Kanye kunyanyuka na kumsogelea Van, lakini nadhani ingekuwa ni mimi asingejaribu hata kunisogelea ningemvujisha damu, kwani ningemsubiria anakuja na ningemrudisha kwa masumbwi, alistahili kipigo“amesema Tyron kwenye mahojiano yake na TMZ Sports kwenye promo ya msimu mpya wa kipindi chake cha The Hollywood Beatdown.

Kwa upande mwingine Tyron amesema kuna vitu ambavyo waandishi wa habari wa kisasa wanapaswa wajifunze ishu kama ya ulinzi binafsi akitolea mfano wa tukio la Kanye West ambaye alinyanyuka kwenye kiti na kumsogelea mtangazaji akitaka wapambane.

Kanye West kwenye mahojiano hayo alinyanyuka kwenye kiti na kuanza kujibizana na Van huku akisikika akisema “unataka kupambana na mimi? sawa ila mimi nakupenda, na kama upo tayari njoo upambane na mimi.“.

Tazama video ya mahojiano hayo hapa chini (video by TMZ).

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents