Burudani

Burna Boy ana jambo lake

Mkali wa Afrobeat kutoka Nigeria Burna Boy amedai kuwa ngoma yake ijayo itakuwa ngoma bora kushinda ngoma zote zilizotoka mwaka huu.

Mwanamuziki huyo ameyasema hayo kwenye mahojiano yake wakati alipokuwa kwenye mahojiano yake wakati alipokuwa kwenye onyesho la mitindo la “Paris Fashion Week” ambapo aliweka wazi kuwa nyimbo ameirekodi siku mbili zilizopita huku akiamini kuwa ndio itakuwa bora kushinda zote.

Kwa sasa Burnaboy anatamba na ngoma ya TshwalaBam Remix aliyoshirikishwa na TitoM na Yuppe ambapo mpaka kufikia sasa ina zaidi ya watazamaji milioni 7.9 kupitia mtandao wa Youtube.

Katika onyesho hilo la mtindo lililofanyika jana jijini Paris nchini Ufaransa mwanamuziki huyo alifanikiwa kutumbuiza ngoma zake mbalimbali ikiwemo Tshwala Bam Remix kwenye Party iliyoandaliwa na Paris Fashion Week.

Mastaa wengine ambao walifanikiwa kuhudhuria katika maonyesho hayo ni Rema, Wizkid, Maluma na Swae Lee na wengineo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents