Habari

Cardi B atangaza rasmi kuhamia Nigeria endapo vita ya Marekani na Iran itaanza, Aahidi kuwashawishi na wasanii wengine

Msanii Cardi B atangaza rasmi kuhamia Nigeria endapo vita ya Marekani na Iran itaanza

Kutokana na machafuko yanayoendelea nchini Iran baada ya Jenerali wa taifa hilo kuuliwa Qasem Soleimani huko katika mji wa Baghdad nchini Iraq wakati anatoka katika uwanja wa ndege.

Baada ya mauaji ya Jenerali huyo raia wa Iran wamekuja juu hadi viongozi wa taifa hilo kutokana na mauaji ya kiongozi huyo ambaye walikuwa wanamtegemea sana na alikuwa anakubalika katika mataifa ya mashariki ya mbali.

Taifa la Iran baada ya kumpumzisha kiongozi wao huyo pendwa katika makazi yake ya milele walitangaza hali ya hatari na taifa la Marekani taifa ambalo lilihusika moja kwa moja katika mauaji ya kiongozi huyo wa Iran baada ya kutuma ndege zisizokuwa na abiria na kumshmbuliwa akiwa pamoja na baadhi ya viongozi wenzake na wasaidizi wake.

Rais wa Marekani Donald Trump alisema kuwa yeye haogopi na endapo Iran wataleta chokochoko basi hatasita kuwashambulia kwani taifa lake la Marekani lina silaha za kutosha na za gharama sana.

Kutokana na kauli hiyo baadhi ya wasanii kutoka Marekani wameonyeshwa kukerwa na kauli hiyo ya Trump na badala yake wameanza kutangaza kutafuta urai wa nchini mbili yaani kutafuta urai wa baadhi ya mataifa ya Afrika.

Miongoni mwa wasanii hao ni Rapper wa kike mwanadada Belcalis Marlenis Almánzar alimaarufu Cardi B ambaye ametangaza kuhamia nchini Nigeria na kuongeza kuwa ataendelea kuwashawishi baadhi ya wasanii wenzake kuhama Mareknai.

Mbali na Cardi B kuchukua uamuzi huo wa kuhamia Nigeria na kuahidi kuendelea kumshawishi mume wake Offset kuondoka nae kitu ambacho kinaelezwa huenda kundi lote la Migos likaamua kuhamia Nigeria kwa kuwa inaelezwa wasanii wote wanaounda kundi la Migosi yaani Offset, Stoff, na Quavo ni ndugu.

Ikumbukwe kuwa mapema mwaka 2019 muigizaji mkubwa kutoka nchini Uingereza Idris Alba alitangaza kuchukua uraia wa nchi mbili ambako alipata uraia wa taifa la Sierra Leone. Mbali na Idris kuchukua urai wa Siera leone pia Rapper na muigizaji mkubwa kwa sasa ambaye ni miongoni mwa waigizaji wanaigiza katika movie ya Fast & Furious Ludacris ambaye ameamua kuchukua urai wa Gabon taifa ambalo anatoka mke wake.

Kwa namna hiyo huenda tukaona wasanii wengi wakichukua urai katika mataifa mbalimbali ya Afrika.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents