Burudani

Diamond Platnumz atangaza ziara yake ya muziki nchini Marekani

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ametangaza ziara yake ya muziki nchini Marekani ambapo atatumbuiza kwenye majiji 12 nchini humo.

Ziara hiyo inayoanza tarehe 22 June hadi 23 July 2018, Diamond atawapagawisha kwa burudani wakazi wa Majiji ya New York, Los Angeles, Minnesota, Houston, Seattle, Kansas City, Washington DC, Boston, Atlanta, Columbus, Philadephia, Dallas.

Kuelekea kwenye Kuachiwa Rasmi kwa Albam ya #AboyFromTandale Ndugu zangu Mlio Marekani Jiandaeni kwa Ziara ya #AboyFromTandaleUSATour mdani ya State hizo 12 kuanzia tareh 22/06 hadi 23/07 Mwaka 2018!!“amesema Diamond Platnumz.

Ziara hiyo ya ‘A Boy From Tandale’ itakuja baada ya kuachiwa kwa album yake ya ‘A Boy From Tandale’ mwezi Machi 14, 2018.

Soma zaidi – Diamond Platnumz asogeza mbele tarehe ya kuachia album yake ‘A Boy From Tandale’

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents