BurudaniHabari

Diamond, Harmonize na Marioo waongoza kusikilizwa

Mwaka 2022 umekuwa mwaka mzuri kwa tasnia ya muziki wa Tanzania, tukishuhudia kuibuka kwa wasanii mbalimbali wanaochipukia, wasanii wakijituma zaidi ya kawaida kwenda kwenye viwango vya juu na kutambulika kimataifa. Mwaka umeshuhudia wasanii takriban sita wa Tanzania wakijiunga na ‘Boomplay Golden club’. Hii ni klabu mahususi kwa wasanii waliopata wasikilizaji zaidi ya milioni mia moja Boomplay huku Tanzania ikiwa nchi ya pili kwa kuwa na wasanii wengi baada ya Nigeria.

Katika kufunga mwaka huu mzuri katika tasnia ya muziki, App namba moja kwenye utoaji wa huduma ya kusikiliza na kupakua muziki barani Afrika, Boomplay, imetoa takwimu zake za kila mwaka ambazo zimekuwa zikisubiriwa kwa hamu. #BoomplayRecap2022 hutoa muhtasari wa matumizi ya muziki na uchambuzi kuhusu ladha na machaguo ya wasikilizaji ndani ya mwaka. Pia, huwawezesha watumiaji wa App kupata orodha zao binafsi za nyimbo bora, wasanii, albamu na aina ya muziki.

Wasanii wa Kiume walioongoza 2022
1. Diamond Platnumz
2. Harmonize
3. Marioo

Wasanii wa Kike walioongoza 2022
1. Zuchu
2. Nandy
3. Maua Sama

Nyimbo zilizoongoza kusikilizwa 2022
1. Nakupenda-Jay Melody
2. Naogopa-Marioo ft Harmonize
3. Utu-Alikiba

Wasanii walioshamiri 2022
1. Jay Melody
2. Marioo
3. Phina

Albamu zilizoongozwa kusikilizwa 2022
1. First of All-Diamond Platnumz
2. Love Sounds Different-Barnaba
3. Only One King-Alikiba

Nyimbo zilizoongoza kwenye chati
1. Naogopa-Marioo ft Harmonize
2. Nakupenda-Jay Melody
3. Utu-Alikiba
Itazame Orodha kamili hapa:-

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents