Habari

Diamond na Rayvanny kutumbuiza Wasafi Festival Kenya, wafunguka makubaliano yao na BASATA (+video)

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ameahidi kufanya show ya karne nchini Kenya katika miji ya Mombasa na Nairobi kupitia tamasha lake la Wasafi Festival 2018.

Akiongea na Waandishi wa Habari Jijini Nairobi leo Desemba 21, 2018 Diamond amelishukuru Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) kwa kumruhusu kufanya tamasha hilo nje ya nchi pamoja na yeye kutumbuiza.

Tarehe 26 tutakuwa Mombasa katika Wasafi Festival, nakuja na niko vizuri Mombasa watafurahi sana. Tarehe 31 Desemba tutakuwa hapa Nairobi watu watafute tiketi mapema kwani najua watu watajaa sana. Kingine niishukuru sana My Government na Baraza langu la sanaa (BASATA) kwa kutupa nafasi hii tena, kutupatanisha na kufanya hizi show, kwa sababu inaonesha ni kiasi gani inasapoti muziki wa Tanzania inatupenda na inapenda tufanye vitu vilivyo bora,“amesema Diamond Platnumz.

Mbali na maelezo hayo Diamond amesema kuwa, licha ya kukubaliwa kufanya tamasha hilo na wao kutumbuiza nje ya nchi. Kuna vitu ambavyo wakimaliza show hizo Kenya watakaa na BASATA kujadili zaidi.

BASATA wiki hii walitangaza kumfungia Diamond na Rayvanny kutofanya show ndani na nje ya nchi.

Kwa upande mwingine, BASATA walitangaza pia kufuta kibali cha usajili wa tamasha la Wasafi Festival .

Hata hivyo, BASATA hawajatoa taarifa rasmi kuhusu kutenguliwa kwa adhabu hiyo, kwa wasanii hao kuendelea na tamasha hilo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents