Michezo

Diarra awatekenya Yanga

Yanga sasa iko mezani na Menejimenti ya kipa Djigui Diarra, ili kumuongeza mkataba mpya wa mwaka mmoja aendelee kuitumikia, licha ya kubakiza mwaka katika mkataba wa sasa. . Kipa huyo raia wa Mali alisaini mkataba wa miaka mitatu na Yanga unaomalizika mwishoni mwa msimu ujao. Mabosi wa Yanga wamekaa mezani na kipa huyo ili kumuongezea mkataba huo mpya kupunguza presha ya alionao utakapomalizika mwakani.

Hata hivyo, pande hizo mbili kati ya Yanga na uongozi wa mchezaji huyo unaonekana bado haujafikia makubuliano kwani bado Diarra hajasaini mkataba huo ikielezwa anataka kuongezewa masilahi apewayo kwa sasa. .

Meneja wa kipa huyo, Djally Tchumbi efunguka kuwa, Yanga bado inataka kubaki kwa muda mrefu na kipa huyo na sasa wako katika mazungumzo yanayoelekea mwisho na mambo yakijiseti Diarra atasaini kwani bado hata yeye anapenda kuendelea kuitumikia.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents