Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemkabidhi Mama Salma Kikwete Nishani ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambayo aliipokea kwa niaba ya Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali ya awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwenye hafla iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma April 24, 2024.
Nishani ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere hutunukiwa kwa Wakuu wa Nchi Wastaafu (hai au marehemu) wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walioingia madarakani kwa njia ya kikatiba na wameendelea kuonesha Maadili mema yenye nidhamu, heshima na mfano wa kuigwa.
Imeandikwa na Mbanga B.