Burudani

Dudubaya awachana BASATA, Atoa msimamo wake juu ya utawala wa Rais Magufuli

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Dudubaya amesema hajapendezwa na tabia ya Baraza la Sanaa Tanzania la kufungia fungia kazi za Wasanii kwa vigezo vya kukiuka maadili.

Dudubaya

Dudubaya amedai BASATA wamekuwa wakifungia kazi za wasanii ambazo tayari zimeshatoka na zimeanza kutumika kitu ambacho kinaonekana kama msukumo kutoka kwa watu.

Dudubaya amesema BASATA wamekuwa wakitoa maamuzi hayo kwa kukurupuka na sio kwa kufuata taratibu kama inavyotakiwa.

Kwa upande mwingine Dudubaya ameweka wazi msimamo wake kuhusu  utawala wa Rais Magufuli, ambapo amesema anapendezwa na maamuzi yake ya kuzuia wasanii wa kike kuvaa nguo za ajabu kwenye video. Msikilize hapa chini akifunguka zaidi

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents