Michezo

Fredy aondoke au abaki?? – Edo Kumwembe

Fredy Michael, rafiki yangu Ahmed Ally wakati akijitamba na vifaa ambavyo vilitua Januari alimpachika jina la ‘Fungafunga’. Wakati huo tulikuwa hatujamuona uwanjani. Jina lilitokea mazoezini. Kama sio mazoezini basi alikuwa amelichukua kutokana na mabao aliyofunga Zambia. Baada ya hapo Fredy ametuchanganya akili. Kila tulipomuona uwanjani alituchanganya akili. Mpaka nyakati hizi nikiwasikiliza Wanasimba wenyewe wanajikuta wamechanganyikiwa kwa Fredy, hasa nyakati hizi ambazo Simba inataka kutoa ‘Thank You’ kwa wachezaji wake.

Fredy aondoke au abaki? Kuna Wanasimba wanasema aondoke kuna ambao wanataka abaki. Tunaishi katika dunia ya namba. Kule alikoondoka amebakia kuwa mfungaji bora na hapa nchini tangu afike amefikisha mabao kumi katika michuano yote. Sio haba. Mara ya kwanza nilipomuona Fredy sikuona kama mshambuliaji wa maana. Lakini anafunga. Hapo ndipo anaponifunga mdomo. Mara ya pili nilipomuona sikuona kama alikuwa mchezaji tishio lakini alifunga. Kuna mechi anacheza ovyo anatukanwa kuliko mchezaji yeyote uwanjani lakini mechi inayofuata anafunga

Wakati mwingine nilikuwa namtazama na kuanza kuhoji ubora wa Ligi ya Zambia. Ilikuwaje akawa anacheka na nyavu pale Zambia mpaka ikafikia hatua ya kuwa mfungaji bora wakati Simba ilipokuwa inamchukua. Na hapo hapo unawaza namna ambavyo hata washambuliaji wengine wa Ligi hiyo walishindwa kumfikia wakati alipoondoka. Tumeanza kuwaacha Wazambia kiuwezo?

Kati yake na Pah Omary Jobe unaona wazi kwamba tofauti yao ni mabao. Hauwezi kuwaamini kama washambuliaji lakini kinachomtofautisha Fredy na Jobe ni kwamba Fredy anafunga. Na sasa ametuachia mtihani wa kukata jina lake. Unajaribu kuangalia na kujiuliza, Simba wapo tayari kuusaka ubingwa wa Afrika huku mshambuliaji akiwa Fredy?” — Edo Kumwembe

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents