Michezo

Giroud afunguka kilichomvutia kujiunga Chelsea

Klabu ya Chelsea imefanikiwa kunasa saini ya mshambuliaji wa Arsenal, Olivier Giroud.

Olivier Giroud

Raia huyo wa Ufaransa amesaini na Chelsea mkataba wa miezi 18 kwa dau la pauni milioni 18 na amekabidhiwa jezi namba 18 .

Kupitia tovuti ya klabu ya Chelsea Giroud amesema amefurahi kujiunga na Chelsea kwani ni moja ya timu zilizochukua makombe mengi ndani ya miaka sita hivyo anaamini na yeye endapo akifanya kazi kwa juhudi ataisaidia klabu hiyo kuongeza mataji.

“Chelsea ni moja ya timu kubwa zinashiriki ligi kuu England, na huenda ikawa ndiyo timu iliyochukua makombe mengi zaidi ndani ya miaka 6 au 7 nafurahi kujiunga nayo na sasa nasubiri kuitumikia zaidi kuleta mafanikio,” amesema Giroud.

Giroud (31) ameondoka Arsenal masaa machache yaliyopita baada ya klabu hiyo kumsaini Pierre-Emerick Aubameyang kutoka Borussia Dortmund.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents