Burudani

Harmonize kesho kuitikisa Dar, Atapiga show na wasanii 11 kiingilio bure (+Video)

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Harmonize kesho Alhamisi Oktoba 31, 2019 atawaburudisha mashabiki wake na watu wanaopenda muziki wa Bongo Fleva bure katika viwanja vya Zakhem-Mbagala jijini Dar Es Salaam.

Kwenye show hiyo ya utambulisho wa hit song yake mpya ya UNO utakuwa na orodha ndefu ya wasanii wa Bongo Fleva akiwemo Maua Sama, -Chief,  Mzee wa Bwax, Linah, Msaga Sumu, Quick Rocka, Mimi Mars, Young Lunya, Country Boy na wengineo.

Huu ni muendelezo wa utambulisho wa wimbo wake wa UNO ndani ya Jiji la Dar Es Salaam, Ambapo ameshafanya hivyo kwa wilaya ya Ilala na baadhi ya nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Kenya na Uganda.

Sikiliza wimbo huo hapa chini;

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents